Teen Talents Tanzania inawakaribisha vijana wote wanaopenda kukuza na kuendeleza vipaji vyao.

Monday, May 21, 2012

TEENTALENTS MODELS FLAVIANA MATATA NI MFANO WA KUIGWA  HUYU NI DADA YENU ALIYE WATANGULIA KUIONYESHA JAMII KIPAJI CHAKE NA ATAISAIDIA VIPI JAMII NA TAIFA KUPITIA KIPAJI CHAKE NA NAFASI ALIYONAYO KATIKA JAMII HII NDO MAANA YA KUA KIOO CHA JAMII.




Historia imewekwa leo na Flaviana Matata alipokabidhi msaada wa maboya (life vests) 500 kwa Shirika la Meli la Taifa (Marine Services Co Ltd) kama sehemu ya kumbukumbu ya MV Bukoba - ambapo ni miaka 16 tokea meli hiyo ilizama na kuua watu takriban 1,000 akiwa pamoja na mama yake Flaviana

Flaviana Matata wakati wa hotuba Baada ya makabidhiano ya maboya na Shirika la Meli la Taifa (Marine Services Co Ltd),alishindwa kuendelea na hotuba yake baada ya kuzidiwa na majonzi ya kumkumbuka mama yake mzazi aliyempoteza katika ajali ya MV Bukoba miaka 16 iliyopita



Flaviana Matata akiweka shada kwenye kaburi isiyo na jina Igoma jijini Mwanza kama sehemu ya kumbukumbu ya watu waliopoteza maisha yao katika ajali ya MV Bukoba. Flaviana alimpoteza mama yake mzazi.



  Flaviana Matata akiwasha mshumaa pamoja na Jackie Sikawa Jema Kimbu Maria Sarungi ... kama sehemu ya kumkumbuka mama yake mzazi ambaye alimpoteza katika ajali ya MV Bukoba miaka 16 iliyopita.... RIP mama Flaviana



R.I.P Mama Falaviana Teen Talents Tanzania inatoa pole na inajivunia kwa alichofanya Flaviana Kwa Taifa.


No comments:

Post a Comment