FOOTBALL UNDER 14 AUDITION IN LEADERS CLUB 28TH MAY
Director (sammy) na refa (ahmed) wakikaribisha wachezaji kabla ya mechi kuanza.
Refa akiongozana na wachezaji
refa akielekeza wachezaji jinsi ya kujipanga
Timu (A) wanajiita Tanzania Kids FC.
Tanzania Kids Fc,Director na refa Katika picha ya pamoja.
Timu (B) Wanajiita ABC.
ABC na Director TeenTalents (Sammy) katika picha ya pamoja.
Timu zote mbili Tanzania Kids Fc na ABC katika picha ya pamoja na Director TeenTalents .
Kabla ya kuwaruhusu wachezaji kwenda kupumzika kwenye seat zao kabla ya mechi kuanza, Refa Ahmed aliwapa changamoto ya kupiga dana dana 50 na mshindi atajichukulia elf 4.
BAADA YA CHANGAMOTO KUTANGAZWA WACHEZAJI WALIANZA ZOEZI KAMA IFUATAVYO.
Mshindi alitokea ABC.
BAADA YA DANA DANA WACHEZAJI WALIKARIBISHWA KUKETI NA KUFANYA MAHOJIANO NA TEEN TALENTS CREW,
Lengo lilikua kujua changamoto gani wanazopata,nini malengo yao katika mpira na elimu na wanatarajia nini??
Wachezaji wa tanzania kids fc na mashabiki wao.
Wachezaji ABC na kocha wao hapa walibadilisha jezi kwa mda madai yao zisichafuke kabla hawajaingia uwanjani wasafi.com men.
Refa (Ahmed) akipanga jukwaa la wachezaji mpira na mashabiki.
Ahmed zain ni IT coordinator wa TeenTalents Tanzania kwa siku hii alisimama kama refa.
MAHOJIANO YALIANZA KATI YA TEEN TALENTS NA WACHEZAJI HAWA WADOGO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 14.
Lengo ni kutambua uwezo wa fikra zao na vipaji vyao.
Teen talents iligundua mengi kutoka kwa watoto hawa uwezo wa akili zao, vipaji vyao, malengo yao na nini kinawapa vikwazo?
MECHI ILIANZA KATI YA ABC NA TANZANIA KIDS FC.
Teen Talents Crew Ikiangalia Mechi.
Kuanzia kushoto mwanzo ni felix (Production Officer) Sammy (Director) Hamida (Secretary) mwisho kabisa Salwa (Make up artist)
MAPUMZIKO
Tanzania Kids Fc Team
ABC Fc Team.
KIPINDI CHA PILI
MECHI ILIIISHA ABC WALIIBUKA WASHINDI WA MAGOLI MATATU BILA.
KILICHOFUATA NI MAJONZI KWA TANZANIA KIDS FC NA HASIRA ZA MICHEZO KAMA IFUATAVYO KATIKA PICHA.
Wachezaji walianza kulia.
Director akimbembeleza na kumpa moyo mchezaji wa tanzania kids fc aliposhindwa kujizuia na kulia sana kwa kuchapwa goli 3 - 0.
Baada ya hapo aliteta nao na kuwapa moyo zaidi.
Director akiwasihi kuongeza juhudi na akimpa pongezi kocha wao kua na wachezaji wenye nia na mapenzi na timu yao kiasi kwamba wana uchungu pale wanaposhindwa.
baada ya hapo walifurahi sana na kupata moyo majonzi yakaisha kwa ishara ya umoja na furaha walipeana tano na Director kwa pamoja.
BAADA YA HAPO DIRECTOR ALIWAFATA NA ABC FC KUWAPONGEZA KWA KAZI NZURI.
Wakimsikiliza kwa makini.
Wachezaji wakitoa asante kwa kushiriki.
Baada ya Mahojiano nao walitoa Tano za pamoja Ishara ya ushindi!
HAIKUISHIA HAPO DIRECTOR ALIWAKUSANYA WACHEZAJI WOTE KUWAPATANISHA NA KUWAELEWESHA ULE ULIKUA NI MCHEZO TU WANAOHUDHUNIKA WASI HUDHUNIKE NA WALIO NA FURAHA WAFURAHIE PAMOJA NA WENZAO.
Magoli kipa wa timu zote mbili.
Haya peaneni mikono nyinyi watoto wa baba mmoja taifa moja na mama yenu mama TeenTalents.
walipongezana
waliendelea kupongezana.
Wakaona Mikono pekee haikutosha wakakumbatiana na kupeana pongezi.
MWISHO
ilikua siku nzuri sana na ilipendeza kuona watoto wadogo kama hawa wana vipaji na wanajua kuvitumia kwa nidhamu na upendo wa hali ya juu!!
watoto hawa wanahitaji udhamini wa jezi,mipira na viatu..... ili waendelee kukuza vipaji vyao
kutokana na malalamiko yao kua hivyo ndio vikwazo walivyo navyo kwa sasa.
PAMOJA SISI NA WEWE TUNAWEZA!!
TEEN TALENTS TANZANIA
EMPOWER YOUTH EMPOWER TALENTS!!.